Nilimuua mama yangu! Tafadhali, naomba msamaha, mama'


AFP

CHANZO CHA PICHA,AFP

Susila hakuwa na nguvu ya kulia licha ya uchungu aliokuwa nao.

Hakuwa na nguvu kabisa ya kusema maneno mengine. Sauti yake ikaanza kukata kata. Kwa dakika fulani alikuwa kimya. Nilisikia tu akivuta pumzi kwa muda mrefu.

Susila ni mama na ana miaka 40. Lengo peke yake alilo nalo ni kuhakikisha binti yake wa miaka 12, anapata elimu nzuri. Kazi ya mume wake ilikuwa inahusishwa na afisa wa usalama.

Susila ni mwanamke ambaye muda wake mwingi yuko nyumbani ana mtunza binti yake na mume wake.

Susila ni wa tatu katika familia ya watoto wanne. Baba yake aliaga dunia. Mmoja wa ndugu zake, Aiya, ni mfanya biashara mkubwa na tajiri.

Dada yake mkubwa ni daktari. Wawili hawa waliondoka katika nyumba ya wazazi wao baada ya kuolewa.

Ingawa ndugu wa mwisho bado hajaoa, amelazimika kukodi nyumba kwasababu ya kazi. Susila pia naye alilazimika kuhamia kwengineko na mume wake kwasababu walitaka mtoto wao apate fursa ya kwenda shule nzuri.

Mama pekee ndiye aliyekuwa amesalia nyumbani na Susila akawa amechukua kama jukumu lake kwenda kwenye nyumba ya mama yake kumtunza. Mama yake alipata maumivu ya goti.

"Dada yangu na kaka yangu wao hawawezi kwenda kumuona mama kila mara kwasababu wao wana majukumu mengi zaidi yangu. Ndio sababu nikaamua kuchukua jukumu hilo na ninampenda mama yangu sana tu." Susila amesema.

Kuna wakati ambao Susila alijipata akiwa kwenye simu anazungumza na mume wake Gamini. Alikuwa anakuja nyumbani wikendi pekee.

"Susila, usijali. Nimepata virusi vya corona. Sasa hivi ninakwenda kwenye kituo cha afya kupata huduma kwahiyo, nitalazimika kusubiri kama wiki mbili au tatu ili kuungana nawe tena. Kuwa muangalifu hadi nitakapokuja," Susila asijue kuwa simu ya Gamini ndio ilikuwa ni mwanzo wa ukurasa mpya wa maisha yake.

Gamini alikuwa amelazwa na siku ile gari likaja hadi nyumbani kumchukua Susila na binti yao. Wawili hao wakapelekwa katika kituo cha karantini.

"Mume wangu yuko hospitali peke yake. Mimi na binti yangu tuko kituo cha karantini peke yetu. Mama yuko peke yake nyumbani." Susila alisema.

Getty Images

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Ilichukua siku chache tu kabla ya Susila na binti yake nao kuanza kuonesha dalili za ugonjwa corona. Watu wote watatu wa failia wakawa wanapata matibabu katika vituo viwili tofauti.

Susila anakumbuka mfadhaiko wa akili aliokuwa anapitia zaidi ya maumivu ya mwili na hata ugonjwa wenyewe.

Hata hivyo, wiki ya kwanza Susila alipokuwa hospitali alikuwa na matumaini kwamba atapona haraka na kurejea nyumbani. Wakati huo, Susila akashutushwa zaidi na simu ya dada yake.

"Mama yangu naye pia amepata ugonjwa wa corona. Akapelekwa hospitali akiwa na matatizo ya kupumua. Wewe ndio uliyepata maambukizi haya awali." Huo ndio ujumbe alioupata kutoka kwa dada yake.

Dada yake ambaye ni daktari, pia naye amejua kwamba mama yake amepata maambukizi ya corona.

Susila, wakati huo akiwa yuko kitandani, aliweka mikono yake pamoja na kumkumbuka Mungu wake. "Mungu Wangu, naomba umponye mama yangu ..."bado anakumbuka akimuomba Mungu wake dua hiyo.

"Mama, nishikilie mkono wangu usiuachie"

Licha ya maumivu aliokuwa anapitia, Susila hakuwa na nguvu ya kulia. Lakini maneno ya faraja kutoka kwa binti yake, yalisababisha machozi kumbubujika.

Mbali na hali yake ya afya, Susila ana wasiwasi sio tu kwasababu ya binti yake na mume wake, lakini pia hali ya mama yake. Inaumiza sana moyo.

Susila akiwa na dalili kali za corona, hakusita kumtazama binti yake aliyekuwa anapitia uchungu kweli kipindi kile. Lakini pia kila mara alikuwa anapiga siku kuuliza hali ya mume wake bila kusahau kumjulia hali mama yake kila baada ya saa.

Lakini moyo wake uliumia zaidi baada ya kufahamu kuwa mama yake amehamishwa hadi chumba cha wagonjwa mahututi.

Susila akiwa amelala kitandani na hawezi hata kusongeza mguu huku binti yake nae akiwa hoi kitandani.

"Mama, naomba nishike mkono wangu, usiuachie." Binti yake alimuomba Susila. Susila asijue kwamba pia binti yake ameingiwa na hofu.

Ilichukua siku chache tu kwa virusi hivyo kubadilisha kabisa maisha ya Susila.

Mama yake Susila alifariki dunia kutokana na virusi vya corona na Susila alipewa taarifa.

LAKRUWAN WANNIARACHCHI/AFP via Getty Images

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

"Kwanini huelewi hili wakati dada yako ni daktari?"

"Sijui kilichonitokea wakati ule. Kifua changu, ghafla kilibana. Nilidhani kwamba hata mimi nitafariki dunia. Nikamkumbatia binti yangu kabisa aliyekuwa amelala kitandani," Susila amesema.

"Nilimtunza mama yangu nikiwa hai. Lakini dakika za mwisho sikuwa na bahati ya kuwa naye. Mama yangu alikwenda safari yake ya mwisho akiwa peke yake. Kwa nini iwe hivyo?" Susila anajiuliza.

'Sina nguvu ya kusonga mbele'

Mume wake, Gamini, alikuwepo Susila aliporejea nyumbani na binti yake baada ya kupona maambukizi ya virusi vya corona. Susila hakuwa na nguvu sio za kimwili wala kiakili kuwezesha watatu hao kuendelea kusonga mbele na maisha.

Hata hivyo, kaka zake na dada zake hawakusita kumshutumu. Alishutumiwa mara kadhaa kwamba yeye ndiye aliyesababisha kifo cha mama yake. Ni uchungu ambao alishindwa kuuvumilia.

"Walisema, umemuua mama. Sikuweza kuvumilia hilo. Kwanini unashindwa kuelewa hili lichaya kwamba wewe ni daktari? Nilimuua mama yangu. Tafadhali nisamehe, mama." Susila alikuwa amepandwa na hisia.

Afya ya Susila iliendelea kuzorota. Gamini anasema kuwa ratiba yake ya kila siku ilibadilika kabisa.

"Hajakula chochote tangu asubuhi. Wakati mwingine anakula mara moja tu. Kila wakatia anasema hana njaa. Amekuwa akiamka usiku wa maneno. Gamini anaelezea.

nBila kuendelea kusubiri zaidi, Gamini alitafuta ushauri wa daktari. Awali walidhania kwamba ni madhara ya ugonjwa corona lakini daktari mmoja akaanza kuulizia maisha ya Susila.

Na daktari huyo akabaini kwamba kinachomsumbua ni matatizo baada ya kupata msongo wa mawazo.

Na hitimisho lake ni kwamba Susila alikuwa amepata ugonjwa wa sonona.

'Namuogopa mama yangu'

LAKRUWAN WANNIARACHCHI/AFP via Getty Images

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

"Corona iliharibu maisha yangu. Tulikuwa familia yenye furaha. Binti yangu ni mzuri sana katika masomo yake lakini sasa elimu yake imetatizika. Kazi yangu pia imenichokesha. Susila alimpoteza mama yake lakini pia alipoteza ndugu zake vilevile." Gamini amesema.

Binti yao wa miaka, 12. Pia naye amekuwa na taharuki. "Namuogopa sana mama yangu. Kila wakati huwa anaangalia juu mbunginu na kusema 'Tafadhali, mama nisamehe'," binti yake alisema.

"Mtu ambaye mwili wake umekuwa dhaifu anaweza kupata ugonjwa wa sonona haraka sana. Hiki ndio kipindi ambacho mtu anahitaji kupata upendo na mapenzi tele badala ya kuwatenga na kuwalaumu. Mtu yeyote anaweza kupata virusi hivi." Dkt. Ramani Ratnaweera, daktari wa magonjwa ya akili, amesema.

Comments