Askofu Gwajima agoma kukaa kwenye kiti alichoandaliwa



Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amegoma kukaa kwenye kiti alichoandaliwa na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka na kupewa kiti kingine kama alivyoomba.

 Askofu Gwajima ameingia kuhojiwa na kamati saa 8:43 mchana huku akigoma pia kutumia kipaza sauti kilichokuwa kimeandaliwa kwa ajili yake.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel Mwakasaka alikubali ombi lake na kubadilishiwa kiti na kipaza sauti

Comments