Atuhumiwa kumuua mtoto wa kaka yake kisha kumtoa viungo vya mwili



Na John Walter-Manyara.

Taarifa ya kusikitisha ya tukio la kikatili kutoka wilayani Mbulu inaeleza kuwa, Mkazi mmoja wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu mkoani Manyara, Harold Hhando anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Emmanuela Hhando (13) na kumtoa viungo vya mwili.

Inadaiwa Hhando alimuua mtoto huyo kwa kumpasua katikati ya miguu na kumtenganisha vipande viwili kisha kukata sehemu za siri, kumtoa maini na kutaka kuyapika ili ayale.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marrison Mwakyoma, amesema tukio hilo lilitokea siku ya jumapili agosti 22,2021 kijijini hapo.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina.

Ameeleza  kwamba walipomhoji mtuhumiwa Hhando alieleza kuwa akiwa ndotoni aliambiwa na mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi.

 

Comments