Gunners 'iko katika kipindi kigumu ambacho hakijawahi kutokea', asema Mikel Arteta


 


Arsenal iko katika 'kipindi kigumu ambacho hakijawahi kutokea hapo kabla', baada ya kuweka rekodi ya kuanza vibaya zaidi msimu huu, kulingana na Mikel Arteta.

Baada ya kufungwa 2-0 na Brentford na sasa Chelsea, Arsenal imepoteza michezo yao miwili ya kwanza ya ligi bila kufunga kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Kikosi cha timu hiyo kimekumbana na ugonjwa wa corona na majeraha katika kipindi cha wiki mbili za ufunguzi.

"Sidhani kama katika historia ya kilabu imewahi kukumbana na kitu kama hiki", bosi Arteta aliambia BBC Sport.

"Lazima tukabiliane na changamoto hii. Ligi au jedwali hakuamuliwi mwezi Agosti. Jambo baya zaidi unaloweza kufanya ni kukata tamaa. Hakika hatutafanya hivyo".

Romelu Lukaku - kwa mara yake ya kwanza kujitokeza tangu ajiunge na Chelsea kwa pauni milioni 97.5 - na Reece James walifunga magoli hayo na Blues walikuwa na uwezo wa kuongeza magoli zaidi.

Mwisho wa siku, Arsenal ilipo ni kati ya wakushukishwa daraja - ukiondoa siku ya ufunguzi wa msimu - ikiwa ni mara ya kwanza tangu Agosti 1992.

"Arteta aliongeza: "Lazima uelewe hali tuliyonayo. Tunakosa wachezaji tisa, na ni vigumu. Sio wachezaji tisa tu - kuna baadhi ya wachezaji wakubwa wakubwa pia".

Walikuwa bila nyota wao wawili katika safu ya washambuliaji - Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette - pamoja na Willian na mlinda mlango Alex Runarsson kwasababu ya ugonjwa wa corona wakicheza dhidi ya Brent

Aubameyang alikuwa amerudi benchi wakati wa mechi dhidi ya Chelsea, lakini beki wa kati wa pauni milioni 50 Ben White alikuwa nje baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Thomas Partey, Gabriel na Eddie Nketiah wote hao pia wamejeruhiwa.

"Lakini pia kuna mengi mazuri", Arteta alisema.

"Wachezaji watano ambao wana umri wa miaka 19 au 20 wanacheza katika kiwango hiki kwa mara ya kwanza - hiyo ni hatua nzuri lakini kwa sasa ni kipindi kigumu". "Lakini sipendi kujihurumia".

Nadhani kila mtu anaweza kuona kwa sasa hatuna kikosi tunachotaka na hali inaonekana kuwa ngumu zaidi kila uchao. "Arsenal walizomewa mbele ya umati wao mkubwa katika siku 533 - lakini Arteta hakuwa na shida na hilo.

"Umati ulikuwa nyuma ya timu tangu mwanzo", alisema.

"Unapopoteza mchezo huwezi kutarajia kwamba watafurahia. Wametoa ushirikiano wao wote walioweza. Tusiposhinda, lazima waonyeshe hivyo na hiyo ni kawaida".

Comments