Posts

DPP: Atakaye vuruga amani ya nchi atashughulikiwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, amesema yeyote mwenye mwenye lengo la kuvuruga amani ya nchi atashughulikiwa bila kujali cheo, jinsia wala dini katika kipindi cha uchaguzi na hata baada ya uchaguzi. Amesema hayo wakati akizindua Ofisi ya Taifa ya Mashtaka wiliya ya Mufindi, mjini Mafinga, ambapo amesisitiza kuwa jukumu la kulinda amani ya nchi ni jukumu la kila mtanzania. ”Ni vizuri kulinda amani tuliyonayo kwasababu machafuko yakitokea tutaenda wapi? nchi nyingi zinataka tuharibikiwe kwasababu wao wameshaharibikiwa hivyo ni vyema taratibu na sheria za nchi tulizojiwekea tuzifuate” DPP Biswalo Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Wiliamu amewataka wananchi kuitumia ofisi hiyo kupata haki na kulinda amani ya eneo hilo kwa maendeleo ya Taifa.

Kiwanda cha Samaki Sumbawanga Kuinua kipato cha wavuvi na kuongeza ajira

Vijiji vitatau Makete vyakabidhiwa hati miliki ya ardhi za kimila

Ujenzi Wa Msikiti Wa Chamwino Dodoma Ulioahidiwa Na JPM Waka

Rais Dkt.Magufuli azungumza na Askofu Mkuu wa KKKT Dkt.Shoo