Maambukizi mapya ya Covid-19 yavunja rekodi Ujerumani, Marekani

 

 


Kwa mara ya kwanza tangu janga la virusi vya corona kuripotiwa nchini Marekani, nchi hiyo imesajili visa zaidi ya 90,000 vya maambukizi ya virusi hivyo katika muda wa siku moja. 

Kulingana na takwimu za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins cha mjini Baltimore, katika muda wa saa 24 zilizopita, watu waliothibitika kuambukizwa virusi vya corona nchini Marekani ni 91,295. 

Chuo kikuu hicho kimesema maambukizi hayo mapya wamefikisha jumla ya watu milioni 8.94 waliokwishapata maambuki ya Covid-19 nchini humo. 

Nchini Ujerumani nako, Taasisi ya Robert Koch inayoshughulikia janga la Covid-19 imesajili maambukizi mapya 18,681, ikiwa ndio idadi kubwa zaidi kuwahi kusajiliwa kwa siku moja. 

Kulingana na taasisi hiyo, karibu watu 500,000 wameambukizwa virusi vya corona kote Ujerumani, na miongoni mwao 11,349 wamekwishaaga dunia.


Comments