Israel inaonekana kuelekea katika uchaguzi wake wa nne katika muda wa miaka miwili baada ya juhudi za mwisho za kuzuia kuvunjwa kwa bunge kushindwa.Mazungumzo yaliyofanyika mapema jana Jumanne yaliyolenga kuleta maelewano juu ya bajeti kati ya vyama vikuu viwili vilivyounda serikali yalikosa kufaulu.
Wanachama wa vyama vya Likud na Bluu na Nyeupe walipiga kura dhidi ya pendekezo la kuahirisha kwa wiki mbili zaidi kupitishwa kwa bajeti ambayo muda wake wa mwisho ilikuwa ni Jumanne.Iwapo serikali itashindwa kupitisha bajeti kufikia usiku wa leo, sheria ya Israel inaeleza kuwa lazima bunge livunjwe na uchaguzi ufanyike katika muda wa siku 90.
Chama cha Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu cha Likud pamoja na chama cha Bluu na Nyeupe chake Waziri wa Ulinzi Benny Gantz zimekuwa vikizozana kuhusu bajeti ya kitaia tangu kuanzishwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa mwezi Mei.

Comments
Post a Comment