Rais wa Uturuki ampokea Waziri wa Afghanistan

    


Rais Recep Tayyip Erdoğan amempokea Waziri wa Uchukuzi wa Afghanistan Kudretullah Zeki.

Waziri wa Uchukuzi na Miundombinu wa Uturuki Adil Karaismailoğlu pia alikuwepo kwenye mapokezi katika Ikulu la Rais.

Kwa upande mwingine, "Mkataba wa Makubaliano juu ya Ushirikiano wa Shughuli za Utafiti na Maendeleo katika Nyanja za Usafiri" ulisainiwa kati ya nchi hizo mbili.

Comments