RC Byakanwa amewataka wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kuacha tabia ya kuwafisha watoto wao

  


Na Faruku Ngonyani ,Mtwara

 Wazazi na walezi Mkoani Mtwara wenye watoto walemavu kuacha kuwaficha watoto hao na badala yake wajitikeze ili wawese kupatiwa mahitaji maalum kama ilivyo kwa watoto wengine.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa alipozindua zoezi la uchunguzi na ubainashaji wa watoto wenye mahitaji maalumu uliofanyika shule ya msingi majengo iliyopo Manispaa Mtwara Mikindani.

Lakini pia Byakanwa amechukua fursa hiyo kuishukuru ofisi ya RAIS TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya elimu juu ya kuwa na mpango wa kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wenye umri wa kwenda shule wanafanya hivyo ili waweze kupatiwa haki yao ya msingi ya kupata elimu.

Aidha Byakanwa ametoa wito kwa wazazi na walezi wenye watoto walemavu (wenye mahitaji maalum)kuacha kuwaficha watoto hao badala yake wajitokeze na kuwapeleka shule ili waweze kupata elimu.

Kwa upande wake Afisa elimu Mkoa wa Mtwara Kiduma Mageni amesema kuwa kwa sasa Mkoa wa Mtwara unajumla ya vituo 22 vya shule ya msingi vinavyotoa elimu kwa wanafunzi wa makundi maalum vilivyopo katika halmashauri zote 9 zilizopo Mkoani Mtwara zenye uwezo wa kubeba wanafunzi elfu 45.

Kiduma ameongeza kuwa mpaka sasa kwa Mkoa wa Mtwara unajumla ya wanafuzi 858 wa mahitaji maalum  wanaopata elimu huku wavulana wakiwa 457 na wasichana 401.

Afisa elimu huyo amesema ameongeza kwa sasa Mkoa wa Mtwara unatarajia kuandikisha wanafunzi 1259 wa mahitaji maalum kwa Halmashauri zote 9 zilizopo Mkoani Mtwara.

Comments