''Posta jipangeni'' - Waziri atoa maagizo

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile ameliagiza Shirika la Posta Tanzania (TPC) kuangalia upya muundo wa Shirika hilo pamoja na kurugenzi zake kama vimekaa sawa na kukidhi mahitaji kwa lengo la kuongeza tija, ufanisi na utendaji wa Shirika hilo.

Dkt. Ndugulile amezungumza hayo alipokuwa akifungua kikao kazi cha Menejimenti na Mameneja wa Mikoa yote wa Shirika la Posta Tanzania kinachofanyika kwa siku tatu jijini Dodoma ili kujadili utekelezaji wa majukumu ya Shirika hilo katika ngazi ya Mikoa.

“Mkaangalie upya mgawanyo wa majukumu yenu ili yale yanayoweza kufanyika katika ngazi ya mkoa yafanyike mkoani na yale ya Makao Makuu yafanyikie Makao Makuu, nchi hii ina mikoa 31 jipangeni vizuri kuhakikisha uwepo wa Shirika katika kila Mkoa”, Dkt. Ndugulile.

Aidha, amezungumzia Sera ya Posta kuwa ni ya zamani na Sheria yake sio Rafiki sana kuwezesha Shirika hilo kufikia maono yake na maono ya Wizara.

Amesema kuwa Wizara imefanya mabadiliko madogo ya Sheria ya Posta ili kuongeza ufanisi katika utendaji na kusisitiza ni vema kutumia fursa ya kikao kazi hicho kukusanya maoni ya Sera mpya ya posta inayoenda kutengenezwa pamoja na mabadiliko ya sheria yanayotarajiwa.

Comments