Metacha Mnata atajwa kujiweka kando ndani ya kikosi cha yanga

 

  

 


IMEELEZWA kuwa kipa namba moja wa Klabu ya Yanga, Metacha Mnata amejiweka kando ndani ya klabu hiyo kutokana na matokeo mabovu ambayo yamekuwa yakipatikana ndani ya timu hiyo.

Mnata aliibuka ndani ya kikosi cha Yanga akitokea Klabu ya Mbao FC ambayo kwa sasa inashiriki Ligi Daraja la Kwanza. 

Mnata jana, Machi 7 alikuwa langoni wakati timu yake ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Sare hiyo imewafanya Yanga wabaki nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 50 kibindoni huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya 8 na pointi zake 29.

Bao hilo alilofungwa dakika ya 89 kwa kichwa cha mchezaji wa zamani wa Yanga, Pius Buswita jambo ambalo liliwafanya malengo ya kusepa  jumla na pointi tatu kuyeyuka dakika za lala salama.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh ameweka wazi kwamba bado hajapata taarifa hizo kwa kuwa wachezaji wa Yanga walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars walielekea kambini.

Comments