Manara afunguka kuhusu Bilioni 20 za Mo Dewji


 


Aliyekuwa Afisa habari na mawasiliano wa ya Klabu ya Simba Haji Manara amefunguka kitendo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Simba Mohammed Dewji kuweka rasmi Bilioni 20 ndani ya klabu hiyo kama alivyoahidi.

Kupitia maelezo yake aliyoweka kwenye mtandano wa Instagram Haji Manara ameandika kuwa "Nikisoma baadhi ya Comments zenu toka jana mnauliza Bughatti Mbona husemi kitu kuhusu billioni 20, ndugu zangu kama kuna Muumini namba moja aliyeshiriki kuwashawishi wanasimba wakubali juu ya muundo huu mpya ni mimi"

 "Nilizodolewa sana, nikatusiwa sana na nikagombana na wengi kuhusu uwekezaji huu, iweje nisiunge mkono jambo lenye maslahi kwa Simba na mpira wetu kwa ujumla"

"Na niwaambie jana ni siku kubwa kwangu kwa sababu nililotaka na kulipigania limekuwa, nitaunga mkono kila jitihada za kuifanya Simba iwe kubwa zaidi na zaidi na Insha'Allah wiki hii nitaongea nanyi kuwashukuru".

Mo Dewji aliweka kiasi hicho cha Bilioni 20 siku ya Julai 30 katika mkutano aliowaita waandishi wa habari.

Comments