Mkurabita yatoa mafunzo kwa wakulima ili waweze kutumia ardhi iliyorasimishi kufanya kilimo biashara
MPANGO wa Kurasalimisha Rasimali na Biashara za Wanyonge nchini (MKURABITA) umeshauri wakulima kutumia fursa ya ardhi iliyorasimishwa kujenga mitaji ya kupata mikopo ya kuendesha kilimo biashara ambacho kitawainua kiuchhumi
Kauli hiyo imetolewa leo katika Kijiji cha Ukondamoyo ,wilayani Sikonge na Meneja Urasilimishaji Ardhi ma Rasilimali vijijini kutoka Ofisi ya Rais ,MKURABITA Anthony Temu wakati wa utoaji wa elimu ya kuwajengea uwezo Wakulima waliorasimisha ardhi zao.
Alisema baada ya kuwajengea uwezo wanalenga kuwaunganisha wakulima waliorasimishiwa ardhi zao na Taasisi za fedha ili waweze kutumia hati hizo za kimila kupata mikopo ambayo itawasaidia kuondokana na kilimo cha mazoea na kuingia katika kilimo biashara.
"Ndugu zangu msiogope kutumia fursa zinazowafikia kama hii ambapo tayari mnazo hati za kimila ili kukopa kwa ajili ya kubadilisha maisha yenu na kujiletea maendeleo"alisema
Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge,Hussein Mchomvu, aliwataka wakulima kuongeza thamani ya mazao yao mashambani kwa kulima mazao ya kimkakati kama korosho ambalo ni zao la kudumu.
Diwani wa Kata ya Kipanga,Yuda William,alisema tangu zamani wakulima hawajanufaika na ardhi yao na kuwa mafunzo yanayotolewa na Mpango wa kurasimisha rasilimali na Biashara za wanyonge Tanzania utabadilisha maisha yao.
Maafisa kutoka Ofisi ya Rais, MKURABITA wapo mkoani Tabora kutoa mafunzo kwa wananchi vijijini kuhusu mpango huo unavyoweza kubadilisha maisha yao baada ya kurasimisha ardhi yao na kuiongezea thamani.

Comments
Post a Comment