Urembo unazidi kuwa ghali mno huku kila mwanadada akifanya lolote kupendeza na hilo linathibitishwa na msanii Shilole ambaye bado hajapata maamuzi ya nini cha kufanya kuhusiana na mwili wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mara kwa mara Shilole amekuwa akipokea maoni mengi juu ya kuongezeka kwa mwili wake kwa maana ya kuwa mnene huku wengine wakimshauri apungue.
Shishi ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohammed, jana kwenye ukurasa wake huo, aliwataka mashabiki wake kumshauri ni njia ipi atumie kupunguza mwili huo alionao.
“Haya jamani ndugu zangu tuongee pamoja ipi nifanye? Nikapigike GYM kiroho mbaya, Nifanye sajari? Nikate utumbo? Haya twende kazi kitakachokuwa na comments nyingi ndo nitakachofanya” – ameaandika Shilole.
Comments
Post a Comment