Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Wananchi kanda ya ziwa wameshauriwa kuendeleza kufanya utalii wa ndani kwa lengo la kuendela kujifunza na ninjia moja wapo ya kufanya mazoezi ya viungo.
Hayo yamesemwa na Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa kisiwa cha saanane Eva Mallya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amewaomba wananchi katika kipindi hiki cha ugonjwa wa uviko 19 kutembelea hifadhi ya kisiwa hicho ili waweze kufanya utalii na mazoezi ikiwa ni njia moja wapo ya kuepuka misongamano isiyo ya lazima kama wataalam wa afya wanavoelekeza.
Alisema ni vema watu kutembelea kisiwa hicho ili waweze kukaa sehemu yenye utulivu ambayo haina msongamano na kujiepusha na maambukizi ya uviko 19 na kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo wanyama.
"Idadi ya wageni iliongezeka kwa mwaka wa fedha uliyoisha 2019/20 kwani zaidi ya watu elfu kumi walitembelea hifadhi hii na mwaka wa fedha uliyoisha 2020/2021 idadi iliongezeka kwa asilimia 30 na kufikia wageni 19,132 kwa sababu ya jitihada za kuhamasisha utalii wa ndani na watu kutambua umuhimu wa kufanya mazoezi na utalii wa ndani sanjari na kuunga jitihada za Serikali.
"Kauli mbiu ya Wizara kwa sasa inasema tumelithishwa tuwalisishe hivyo ni vema kila mmoja kufanya utaliia ili aweze kufadi tulichopewa na mungu wetu,"alisema Mally.
Kwa upande wake Afisa Uhifadhi wanyamapori Mkuu wa kitengo cha Utalii wa hifadhi hiyo Hilda Mikongoti alisema kwenye hifadhi hiyo kuna wanyama mbalimbali wakiwemo simba,Swala, pimbi,Tumbili,Digidigi,Fisi Maji,Nyumbu,Pundamilia,Mamba Ndege na michezo ya watoto.
" kwenye hifadhi hii kuna michezo mbalimbali ya Watoto kwani wanaweza kubembea huku wakiangalia wanyama kwa sababu wapo karibu na nirahisi kupiganao picha,"Mikongoti
Alisema hifadhi hiyo ambayo ipo ndani ya ziwa victoria ina vuvitio mbalimbali kwani unaweza kutalii Kwenye ziwa Kwa kutumia boti kuangalia mandhari mazuri yanayozunguka kisiwa hicho ambacho kimezungukwa na miamba na upepo mzuri.


Comments
Post a Comment