Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amekitaka Chuo cha Misitu Olmotonyi kihahakishe kinawafuata wananchi huko waliko na kuwapa elimu ya kukabiliana na moto kichaa
Ametoa rai hiyo Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na watumishi wa Chuo cha Misitu Olmotonyi ambapo amewataka watumishi hao kutumia ujuzi wao kutoa elimu kwa wananchi kwa kuwafuata huko waliko.
Amesema moto kichaa ni tatizo kubwa katika misitu inayomilikiwa na Serikali pamoja na ile ya watu binafsi
kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro ameutaka Uongozi wa Chuo hicho uhakikishe unawatumia Wakufunzi wake kwenda maeneo mbalimbali ya nchi kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuweza kukabiliana na tatizo la moto kichaa.
Amesema ana amini elimu itakayotolewa na Wataalamu hao itawasaidia wananchi kuweza kupambana na tatizo la moto kichaa ambalo limekuwa likiathiri misitu mingi hapa nchini
Comments
Post a Comment