Dkt.Gwajima amekagua ujenzi wa jengo maalum la mionzi ya saratani katika hospital ya Rufaa Kanda ya kasikazini KCMC
Waziri Wa Afya Maendekeo ya jamii jinsia wazee na watoto Dkt Dorothy Gwajima amekagua ujenzi wa jengo maalum la mionzi ya saratani katika hospital ya Rufaa Kanda ya kasikazini KCMC kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi
Dkt Gwajima amesema kuwa serikali imejipanga kuboresha huduma katika hospitaki za kanda ya kasikazini Kilimanjaro,Mbeya Musoma Mwanza Na Hospirali ya Chato ili kuwapunguzia adha wagonjwa kusafiri kwenda jijini Dar es salaam kufuata huduma ya mionzi.
Amesema kuwa serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imeweka mikakati ya kuboresha huduma za afya mijini na vijijini ikiwemo kujenga majengo maalumu ya mionzi ya saratani ili wagonjwa wapatiwe matibabu kwenye maeneo yao


Comments
Post a Comment