Gari la Mbunge lachomwa moto

 

 

Mariagorreth Charles

29Sep 2021

                                     

 

Kuamkia leo 29/09/2021  watu wasiojulikana wamechoma moto gari la Mbunge wa jimbo la Mbozi George Mwenisongole aina ya Brevis T 231 DDZ.  

Tukiwa hill imetokea  nyumbani kwake Ichenjezya Vwawa Mbozi Songwe.

 

 Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ambae ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ameeleza  kuwa  chanzo cha tukio hilo hakijajulikana upelelezi unaendelea kwa mamlaka husika ya katika kuchunguza tukio hilo.

 

Aidha, Mbunge  Mwenisongole amesikiyishwa na kitengo hicho .

Akizungumza na GORRETH BLOG  amesema kuwa tukio hilo limetokea saa tisa usiku ambapo Majirani walisikia mbwa wakibweka kwa muda wa nusu saa na baadae ulitawala ukimya .

 Ndio walipochukua maamuzi ya kutoka nje na kukuta gari hilo likiteketea kwa moto.

Comments