Mwanamke na mwanaume ni sawa -Rais Samia



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa mwanamke na mwanaume ni viumbe sawa na hivyo wote wana haki sawa katika jamii, mbali na zile haki za Kimungu zilizompa mwanamke mamlaka ya kulea mimba na kuzaa.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 28, 2021, Jijini Dodoma, aliposhiriki katika maadhimisho ya miaka 50 na kongamano la Wachungaji na Maaskofu wa Kanisa la Anglikana.

Comments