Rais Samia aipongeza Wizara ya Afya




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan ameipongeza Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto ķwa kubuni wazo la kufanya mkutano unaohusisha Taasisi za Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali, amesema, mashirika haya yanamchango mkubwa kwa Taifa ikiwemo kutoa ajira kwa vijana.

Pongezi hizo amezitoa Jijini Dodoma katika mkutano wa mwaka wa Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo yamefanya majadiliano ya pamoja hali itakayo ondoa utata na tofauti kati ya taasisi za serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali

Mhe.Rais Samia Suluhu Hassani ambaye ni zao la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambapo amewahi kufanya kazi katika mashirika katika kipindi cha miaka kumi hivyo anaimani kuwa mashirika ya kiserikali yanamchango mkubwa kwa taifa.

Comments