Waziri Gwajima ampongeza Dkt. Nyanga kwa kuteuliwa



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima leo 28/9/2021 amekutana na Dkt. Ali S Nyanga na kumpongeza kwa kuteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kuwa Mkurugenzi wa kinga na elimu ya afya Wizara ya Afya, Ustawi Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Zanzibar.


Aidha kabla ya utezi wa Dkt. Nyanga alikuwa Meneja Uratibu wa Matukio ya Dharura ya Afya kwa Umma WAMJW.

Comments