Moto jirani na hosteli za UDSM wateketeza vibanda vya wafanyabiashara


 

Moto ambao chanzo chake hakijafahamika umeteketeza vibanda vya wafanyabiashara vilivyopo kando ya  barabara ya kuelekea katika hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).


Moto huo ulianza leo Ijumaa Novemba 12,2021 saa 2 asubuhi lakini kikosi cha Jeshi la Zimamoto  na Uokoaji  kilifika eneo hilo kuzima moto huo.


Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Khamis amesema moto umeanzia katika kibanda kimoja cha mama ntilie kabla ya kushika mabanda  mengine.


 "Banda lililokuwa likifuata ni la  kuhifadhia magodoro, ulipoingia ndani ya kibanda hicho uliongezeka na kuwa mkubwa kabla ya kushika banda jingine la kuuza la mbao na kueleke  sehemu ya kuosha  magari," amesema Khamis.


Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Makaburi Kibangu, Moshi Khaftan amesema alipata taarifa ya moto huo ya saa moja na nusu asubuhi  na kupiga simu Zimamoto.


Comments