Manchester City imemuongeza mlinzi wa kushoto wa Tottenham na Italia Destiny Udogie, 22, kwenye orodha fupi ya wachezaji wanaotarajiwa kusajiliwa huku wakipania kuimarisha nafasi ya mlinzi wa pembeni msimu huu. (Fabrizio Romano)
Kocha wa Lens Mwingereza aliyezaliwa Ubelgiji, Will Still, 32, ni miongoni mwa wanaowania kuwa meneja mpya wa Southampton kufuatia kuondoka kwa Ivan Juric mapema wiki hii. (Talk sport)
Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool, Newcastle na Spurs zimekutana au kufanya mazungumzo na wawakilishi wa mlinzi wa Uhispania mzaliwa wa Uholanzi Dean Huijsen, kabla ya uamuzi kufanywa kuhusu hatma ya mchezaji huyo wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 19. (Athletic)
Comments
Post a Comment