MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/21 ambayo inaandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), inatarajiwa kuanza wikiendi hii ikiwa ni mara ya 57 tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo lakini ni mara ya 25 tangu kuanza kutumika kwa mfumo huu unaotumika sasa.
Bingwa wa msimu huu atapata nafasi ya kushiriki mechi ya CAF Super Cup mwakani, pia timu tatu za juu zitafuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia la Klabu nchini China mwakani pia.
Mataifa yanavyotoa timu
Wanachama wote 56 wana haki ya kupata timu shiriki katika michuano hiyo, mashirikisho na vyama vya mataifa 12 ambayo yana viwango vya juu kwa pointi za Caf walizopata ndani ya miaka mitano iliyopita, wanapewa nafasi ya kupeleka timu mbili ndani ya msimu mmoja.
Hivyo kwa mujibu wa hesabu hizo, ni wazi kuwa idadi ya timu shiriki ambazo zinatakiwa kuwemo kuanzia hatua ya awali ni 68 lakini idadi hiyo haijawahi kutimia kutokana na sababu mbalimbali.
Pointi za ubora huwa zinapatikana kutokana na ubora wa timu ngazi ya klabu kwa hatua zinazopitia au kufika ndani ya miaka mitano tangu msimu husika unaotakiwa kufanyika kwa michuano husika.
Utaratibu huu wa kuhesabu pointi pia unahusika hata katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Utaratibu wa pointi za ubora upo hivi…
Ligi ya Mabingwa Kombe la Shirikisho
Bingwa 6 pointi 5 pointi
Wa pili 5 pointi 4 pointi
Nusu Fainali 4 pointi 3 pointi
Robo Fainali 3 pointi 2 pointi
Wa 3 kundini 2 pointi 1 pointi
Wa 4 kundini 1 pointi 0.5 pointi
Ili kupatikana kwa pointi husika kwa taifa, sasa kinachofuata hapo ni kuwa idadi ya pointi zinazidishwa kwa idadi maalum kulingana na miaka ambayo timu zimefika hatua fulani.
Yaani ile timu ambayo au ambazo zimefika hatua ya mbali mwaka jana pointi zake zinazidishwa mara 5, zile za mwaka juzi zinazidishwa mara 4. Mfano kama Tanzania ina pointi 10 kutokana na pointi ilizopata kwa mafanikio ya klabu yake, idadi hiyo inazidishwa mara 5 au 4 au 3 kwa kutegemea na mwaka wa hatua ya mwisho waliyofika katika mwaka wao wa mwisho kushiriki katika michuano.
Hii inamaana kuwa utaratibu huu unakuwa unaendelea hivyohivyo, kabla ya msimu kuanza, mahesabu yanapigwa na ile ambayo imefanya vizuri ndani ya mwaka mmoja uliopita kabla ya michuano husika, inakuwa na nafasi kubwa ya kupata pointi nyingi zaidi.
Mfano wa utaratibu wa pointi zilivyohesabiwa kuelekea kuanza kwa msimu huu upo hivi:
2019–20: x5
2018–19: x4
2018: x3
2017: x2
2016: x1
Timu
Kutokana na janga la Ugonjwa wa COVID-19, mashirikisho na vyama mbalimbali vilisitisha ligi zao na kuamua kuchagua washiriki kwa vigezo vya waliokuwa kileleni kupewa nafasi.
Pointi za ubora wa nchi shiriki
Kuelekea kuanza kwa msimu huu, inamaanisha kuwa mahesabu ya pointi zilipigwa kulingana na ushiriki wa timu kuanzia mwaka 2016 hadi 2020 katika michuano hiyo inayosimamiwa na CAF:
Wanaoingiza timu mbili msimu huu kutokana na pointi zao:
Nchi Pointi Timu shiriki
- Morocco 190 Raja Casablanca, Wydad Casablanca
- Misri 167 Al Ahly, Zamalek
- Tunisia 140 Espérance de Tunis, CS Sfaxien
- DR Congo 83 TP Mazembe, AS Vita Club
- Algeria 81 CR Belouizdad, MC Alger
- Afrika Kusini 68.5 Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs
- Zambia 43 Nkana, Forest Rangers
- Nigeria 39 Plateau United, Enyimba
- Guinea 38 Horoya, Ashanti de Siguiri
- Angola 36 Petro de Luanda, 1º de Agosto
- Sudan 29.5 Al Merrikh, Al Hilal
- Libya 16.5 Al Nasr, Al Ahly Benghazi
Wanaoingiza timu moja msimu huu kutokana na pointi zao:
Nchi Pointi Timu shiriki
- Tanzania 14 Simba
- Ivory Coast 13 RC Abidjan
- Kenya 11 Gor Mahia
- Zimbabwe 11 FC Platinum
- Msumbiji 9 Costa do Sol
- Congo 8 AS Otohô
- Uganda 8 Vipers
- Ghana 6.5 Asante Kotoko
- Mali 6.5 Stade Malien
- Rwanda 6 APR
- Eswatini 5 Young Buffaloes
- Ethiopia 4 Mekelle 70 Enderta
- Botswana 3 Jwaneng Galaxy
- Togo 3 ASKO Kara
- Benin 2.5 Buffles du Borgou
- Mauritania 2.5 FC Nouadhibou
- Burkina Faso 2 Rahimo
- Cameroon 2 PWD Bamenda
- Gabon 1 AS Bouenguidi
Burundi — Le Messager Ngozi
Chad — Gazelle
Comoros — US Zilimadjou
Djibouti — GR/SIAF
Equatorial Guinea — Akonangui
Gambia — Gambia Armed Forces
Lesotho — Bantu
Niger — AS SONIDEP
Senegal — Teungueth
Somalia — Mogadishu City
Zanzibar — Mlandege
Mataifa ambayo hayajaingiza timu msimu huu:
Cape Verde Central African Republic Eritrea Guinea-Bissau Liberia Madagascar Malawi Mauritius Namibia Réunion São Tomé and Príncipe Seychelles Sierra Leone South Sudan.
Ratiba
Michuano imechelewa kuanza sababu kubwa ilikuwa maambukizi ya Covid-19. Mechi za kwanza zitachezwa Novembea 27-29, marudio ni Desemba 4-6, mwaka huu.
Raundi ya Awali
Nov 27-29 & Des 4-6
Raundi ya Kwanza
Des 22-23 & Jan 5-6
Hatua ya Makundi
Februari 12-13, 2021
Februari 23-24, 2021
Machi 5-6, 2021
Machi 16-17, 2021
Aprili 2-4, 2021
Aprili 9-11, 2021
Robo fainali
Mei 14-16 & Mei 21-23
Nusu Fainali
Juni 18-20 & Juni 25-27
Fainali
Julai 17, 2021
Raundi ya Awali ipo hivi…
Kutakuwa na mechi mbili, nyumbani na ugenini, timu zikilingana pointi na mabao, faida ya bao la ugenini itatumika, hapo napo wakilingana watapigiana penalti, hakutakuwa na dakika 30 za nyongeza, lakini wikiendi hii mambo ni hivi:
Ashanti de Siguiri v Stade Malien, Gambia Armed v Teungueth RC Abidjan v ASKO Kara
AS SONIDEP v Mogadishu City
Al Ahly Benghazi v Mekelle 70 Enderta
Gazelle v GR/SIAF
Forest Rangers v AS Bouenguidi
Jwaneng Galaxy v US Zilimadjou
Young Buffaloes v Le Messager Ngozi
PWD Bamenda v Kaizer Chiefs
AS Otohô v Al Merrikh
Rahimo v Enyimba
FC Nouadhibou v Asante Kotoko
Vipers v Al Hilal
Buffles v MC Alger
Mlandege v CS Sfaxien
Bantu v Nkana
Akonangui v Petro de Luanda
Costa do Sol v FC Platinum
Plateau United v Simba
CR Belouizdad v Al Nasr
APR v Gor Mahia
Raundi ya Kwanza
Timu 10 zimeshawekwa katika kundi hili kusubiri zile za Raundi ya Awali, hii ni kutokana na ubora wao waliouonyesha ndani ya miaka mitano iliyopita. Hivyo zitakutana na zile
Ashanti /Malien v Wydad Casablanca
Armed/Teungueth v Raja Casablanca
RC Abidjan/ASKO v Horoya
SONIDEP/Mogadishu v Al Ahly
Al Ahly/Mekelle v Espérance de Tunis
Gazelle/GR v Zamalek
Forest/Bouenguidi v TP Mazembe
Galaxy/Zilimadjou v Mamelodi
Buffaloes/Ngozi v AS Vita Club
PWD/Kaizer Chiefs v 1º de Agosto
Otohô /Merrikh v Rahimo/Enyimba
Nouadhibou/Kotoko v Vipers/Al Hilal
Buffles/MC Alger v Mlandege/Sfaxien
Bantu/Nkana v Akonangui/ Luanda
Costa/Platinum v Plateau/Simba
CR Belouizdad/Al Nasr v APR/Gor Mahia
Na John Joseph
Comments
Post a Comment