Umoja wa Ulaya watoa wito kwa wanachama wake kutosafiri kwenda Uingereza

 

 


Umoja wa Ulaya umependekeza kwa nchi wanachama wake 27 kufuta safari zisizokuwa za lazima za kuelekea Uingereza hadi watakapotoa tangazo lengine.

Kamishna wa sheria wa Umoja wa Ulaya, Didier Reynders, amewatolea wito raia kutoka mataifa wanachama wa Umoja huo kutosafiri kwenda nchini Uingereza kwa sasa.

Hata hivyo, kamishna huyo ameongeza kuwa marufuku ya usafiri iliyowekwa haipaswi kuzuia maelfu ya raia wa Umoja wa Ulaya na Uingereza kurudi makwao.

Licha ya Umoja wa Ulaya kupiga marufuku safari za ndege za abiria kutoka Uingereza kutokana na kuibuka kwa aina mpya ya kirusi cha Corona, Umoja huo umezitaka nchi hizo kuruhusu raia wao kurudi majumbani alimradi waoneshe cheti cha matibabu kutibitisha kuwa hawana maambukizo ya Covid-19.


Comments