ETTIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa bahati ya timu hiyo kuweza kutinga hatua ya robo fainali kwenye michuano ya Chan nchini Cameroon.
Benchi la ufundi la Stars lipo mikononi mwa Ndayiragije ambaye anafanya kazi kwa kushirikiana na Seleman Matola pamoja na Juma Mgunda ambao ni wasaidizi wake.
Ikiwa Cameroon wakati ikishiriki michuano ya Chan ambayo inawahusisha wachezaji wa ndani imefungashiwa virago hatua ya makundi baada ya kukusanya pointi nne kwa kuwa ilishinda mchezo mmoja kwa bao 1-0 dhidi ya Namibia na ilifungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia na ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Guinea.
Mechi ya ufunguzi ilipoteza dira ya Stars kwa kuwa wachezaji walipoteza hali ya kujiamini na alianzisha pia kikosi chenye wachezaji wengi ambao hawana uzoefu na mechi za ushindani.
Miongoni mwa wachezaji ambao walianza kikosi cha kwanza na hajawahi kuwatumia kwenye mechi ngumu ni pamoja na mshambuliaji Yusuph Mhilu, Kalos Protus na Edward Manyama.
Ndayiragije amesema:"Haikuwa bahati yetu kusonga mbele licha ya wachezaji kupambana kusaka ushindi. Pia mwamuzi wa mchezo wetu dhidi ya Guinea alifanya makosa mengi ambayo yametufanya tutolewe,".
Kwenye kundi D ambazo zimesonga mbele ni Guinea na Zambia ambazo zote zimekusanya pointi tano kibindoni.
Comments
Post a Comment