Somalia yatangaza hali ya hatari baada ya nzige kusababisha uharibifu wa mashamba ya wakulima

  


Somalia ilitangaza hali ya hatari baada ya aina mpya ya nzige wa jangwani waliotapakaa eneo la Afrika Mashariki kusababisha uharibifu mkubwa kwa wakulima katika mkoa wa kusini mwa nchi.

Katika taarifa iliyotolewa na runinga ya serikali ya Somalia kupitia akaunti ya Twitter, iliandikwa,

"Wizara ya Kilimo ya Somalia imetangaza hali ya hatari kutokana na uvamizi wa nzige nchini."

Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya mkutano kufanyika kati ya maafisa wa Wizara ya Kilimo, mawaziri wa kilimo wa serikali na maafisa wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FOA).

Mikoa mingi nchini Kenya pia iliripotiwa kuvamiwa na nzige wa jangwani kutoka Ethiopia na Sudan.

Makundi ya nzige ambayo ni tishio kubwa kwa usalama wa chakula, yaliharibu mamia ya maelfu ya hekta za ardhi ya kilimo katika mkoa huo mwaka jana.

Nzige milioni 40-80 katika kilomita moja ya mraba wanaweza kula chakula kinachotosheleza watu elfu 35 kwa siku moja tu.

Makundi hayo ya nzige huweza kusafiri kilomita 150 kila siku.

Comments