Tetesi za soka kimataifa

 

 


Mshambuliaji Lionel Messi, 33, hajafikia mkataba wowote na timu ya Paris St-Germain au Manchester City.

Mkataba wake na Barcelona ambao bado unasifika unamalizika msimu huu lakini atasubiri hadi mwisho wa msimu kuamua ikiwa atasalia kwenye klabu hiyo au atahamia kwengineko. (Goal)

Winga wa Ukraine Marian Shved, 23, amekubali kwamba alifanya makosa kujiunga na Celtic badala ya Genk miaka miwili iliyopita. Shved sasa hivi yuko kwa mkopo Mechelen kutoka Celtic. (Glasgow Live)

Kylian Mbappe anataka kujiunga na Real Madrid, amesema Jese Rodriguez, aliyekuwa mchezaji mwenzake huko Paris St-Germain. (Marca)

Mlinzi wa Serbia Aleksandar Kolarov, 35, na beki raia wa Italia Matteo Darmian, 31, wote wanatarajiwa kuondoka Inter Milan msimu huu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Vilabu sita vya Ligi ya Primia huenda vikacheza katika Ligi ya Mabingwa kuanzia mwaka 2024 kuendelea. Mapendekezo ya Uefa yatawezesha timu kucheza mechi 10 za makundi kila moja huku kukiwa na uwezekano Ligi ya Europa ikapunguza idadi ya timu zitazoshiriki ligi hiyo.

West Ham inatarajiwa kutoa kitita kingine cha pesa kwa ajili ya mshambuliaji wa Sevilla raia wa Moroccan Youssef En-Nesyri, 23, msimu huu. (Star)

Timu kubwa za Ulaya zitapewa fursa ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa hata kama zitashindwa kumaliza katika nafasi ya nne kwenye mashindano yao ya ndani, Uefa imesema hivyo kwa vilabu vya Ligi ya Primia kama moja ya mipango yake. (The Times - subscription only)

Winga wa West Brom Kyle Edwards, 22, alikuwa ndiye anayejadiliwa katika klabu ya Luton Town siku ya mwisho ya uhamisho - lakini makubaliano ya mkopo yalionekana kuwa ya gharama ya juu zaidi. (Birmingham Mail)

Real Madrid inastahili kufikiria kumuuza kiungo wa kati wa Ubelgiji Eden Hazard, 30, amesema aliyekuwa mshambuliaji wa Bulgaria Dimitar Berbatov. (Betfair via Marca)

Blackburn Rovers itatafuta kufikia makubaliano ya muda mrefu na wachezaji wengi wa msingi akiwemo mshambuliaji wa Adam Armstrong, 23, miaka michache ijayo. (Lancs Live)

Aliyekuwa beki wa Manchester United Fabio da Silva ameiambia klabu yake ya zamani kumsajili beki wa kulia mpya ili kumpa msukumo Aaron Wan-Bissaka, 23, wa kufikia viwango vingine. (Manchester Evening News)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal Jeff Reine-Adelaide, 23, huenda akakosa mechi kwa kipindi kirefu baada ya kupata jeraha katika mishipa ya goti lake. Raia huyo wa Ufaransa yuko Nice kwa mkopo kutoka Lyon. (RMC Sport)

Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Uhispania Sergi Roberto, 28, huenda asishiriki mechi katika kipindi cha wiki sita kwasababu ya jeraha ambako kuna maanisha kwamba huenda akakosa mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Paris St-Germain. (TV3 via Mundo Deportivo - in Spanish)

Comments