UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kuna umuhimu wa wapinzani wao Simba kujipanga wakati mwingine ikiwa wataandaa mashindano kama ya Simba Super Cup.
Januari 27 Simba Cup ilianza na ilishirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyewe wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe na bingwa wa mashindano hayo alikuwa ni Simba.
Mechi zote tatu zilichezwa Uwanja wa Mkapa ambapo mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na mechi ya pili iliazimisha sare ya bila kufungana na TP Mazembe.
Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa mabingwa hao wa Simba Super Cup kujipanga wakati mwingine ili kufanya vizuri.
"Ninakubali kwamba wameandaa Simba Super Cup ila ilibidi wajipange na kufanya tathimini wakati mwingine, yaani umechukua kombe mwenyewe, kombe umeliaandaa mwenyewe.
"Upande wa tuzo binafsi nazo pia unajipa mwenyewe kuanzia mchezaji bora wako, mfungaji bora tena mabao yenyewe mawili, haikuwa inahitajika
hiyo iwepo.
"Wajifunze baadaye kwamba sio lazima kuipa timu yako kipaumbele katika mambo ambayo umeyaandaa kisa wewe ni muadaaji," .
TP Mazembe ni mshindi wa tatu na Al Hilal ni mshindi wa pili kwenye mashindano hayo ambayo yalikuwa ni ya kwanza kwa mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck, Didier Gomes.
Comments
Post a Comment