Bunge limeahirishwa hadi Agosti 31 mwaka huu, awataka waende kuhamasisha sensa



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, wabunge pamoja na viongozi wengine kuanza kuwahamasisha Wananchi kujiandaa na sensa ya Watu na Makazi iliyopangwa kufanyika mwezi Agosti mwaka 2022.

Akiahirisha Bunge la 12 jijini Dodoma Waziri Mkuu Majaliwa amesema sensa hiyo ambayo ni ya sita hapa nchini, itaisaidia Serikali kupata taarifa za msingi zitakazosaidia mchakato wa utekelezaji wa dira ya maendeleo ya mwaka 2025, mageuzi ya masuala ya afya na jamii, pamoja na ufuatiliaji wa ajenda za maendeleo za kimataifa.

Ametoa wito kwa Watanzania wote kuanza maandalizi yatakayowawezesha kutoa taarifa sahihi wakati wa sensa hiyo ya Watu na Makazi, huku wakitambua kuwa sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi kwa umri, jinsia na mahali wanapoishi.

Sensa ya Watu na Makazi ni zoezi la kitaifa linalofanyika kila baada ya miaka 10 ambapo sensa ya mwisho kufanyika nchini ni ile ya mwaka 2012.

Comments