Imeripotiwa kuwa Israel italazimika kuharibu dozi 800,000 za chanjo ya corona (Covid-19), ambazo tarehe yake ya mwisho ya matumizi inakaribia, ikiwa hakuna mahitaji kutoka nchi zingine.
Kulingana na ripoti ya Shirika la Utangazaji wa Umma la Israel (KAN), utawala wa Tel Aviv una dozi 800,000 za chano ya Covid-19, ambazo tarehe yake ya mwisho ya matumizi inakaribia.
Ikiwa hakuna mahitaji kutoka nchi zingine, Wizara ya Afya ya Israel italazimika kuharibu chanjo hizi.
Ingawa ripoti haikutaja chanjo ya Israel ni ya kampuni gani, utawala wa Tel Aviv ulinunua chanjo ya BioNTech-Pfizer.
Mnamo Juni 18, Israel ilikubali kubadilishana chanjo za Covid-19 zilizokwisha muda wake na Palestina.
Chini ya makubaliano hayo, Israel ingetoa chanjo zaidi ya milioni 1 za BioNTech-Pfizer kwa Palestina.
Kwa upande mwingine, chanjo ambazo Palestina ingepokea kutoka BioNTech-Pfizer mnamo Septemba na Oktoba zitatumwa kwa Israel.
Mamlaka ya Palestina ilifuta makubaliano hayo kwa madai kuwa tarehe ya kumalizika kwa chanjo zitakazotolewa na Israel ingefika ndani ya muda mfupi.
Comments
Post a Comment