Maandamano ya Sudan yapangwa wakati wa mageuzi magumu ya kiuchumi


 


Miaka miwili baada ya vurugu nchini Sudan kusababisha mwisho wa utawala wa miaka 30, maandamano yanatarajiwa Jumatano katika mji mkuu Khartoum.

Serikali ya mpito imeanzisha mageuzi magumu ya kiuchumi, na imeshinda uungwaji mkono kutoka kwa taasisi za mikopo za kimataifa.

Jumanne, Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) liliidhinisha mkopo wa dola bilioni 2.5bn kwa Sudan.

Lakini mfumko mkubwa wa bei na kukoma kwa ruzuku ya mafuta vimewaacha Wasudani wengi wakitaabika.

Kuna wasiwasi pia kwamba wanajeshi watiifu kwa serikali ya zamani wanatafuta kudhoofisha mabadiliko ya demokrasia.

Comments