Wafanyabiashara watakiwa kujiimarisha na kuongeza uwezo



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR

KATIBU mtendaji wa Idara ya usimamizi wa soko huru barani afrika (AfCFTA) Wamkele Wene amewashauri wafanyabiashara nchini kujiimarisha na kuongeza uwezo wa uzalishaji wa bidhaa na huduma wanazotoa ili kunufaika moja kwa moja na soko la huru barani afrika.

Soko huru barani afrika (AfCFTA) ni makubaliano ya kibiashara ambapo nchi za kiafrika zimekubaliana kufungua mipaka kwa raia wao kuuza na kutoa huduma katika mataifa mengine,hadi sasa nchi 49 tayari zimekubali kungi katika soko hilo.

Wito huo ameutoa wakati akifungua wa mkutano maalumu wa majadiliano ya pamoja juu ya mchango wa sekta binafsi katika soko huru barani afrika (AfCFTA) ambapo mkutano huo umefanyika katika hotel ya Madinat Al Bahr Mbweni Mjini Unguja.

Wene alisema uwepo wa soko huru barani afrika (AfCFTA) kuna fungua fursa za wafanyabiashara kuwa na soka la pamoja la kuuza  bidhaa wanazozizalisha pamoja na huduma wanzitoa.

Alisema kuwa wafanyabiashara na sekta binafsi huu si wakati wa kuogopa wanachotakiwa kuhakikisha wanaridhia kuingia katika mpango wa soko huru la afrika kwani huko kunapatikana fursa mbalimbali kwao.

“Uwepo wa AfCFTA imekuja kuwaweka pamoja waafrika ambapo wafanyabiashara watapata masoko kwa sekta nzima ya binafsi hawatakiwi kuogop kwani kuna taasisi za kifedha zipo wa ajili ya kuwawezesha na kuendana na soko hilo,” alisema.

Alieleza kwamba kupitia soko huru afrika kwa ambazo zitakuwa zimeridhia mkataba wake watapata fursa yakukopeshwa fedha na taasisi za kifedha kwa lengo la kuwakuza wafanyabiashara na kuendana na soko hilo.

Aidha Wakele Wene aliwaasa sekta binafsi kuhakikisha wana wajengea uwezo wafanyabiashara nchini wa kutafuta masoko na kutuma teknolojia.

“AfCFTA, ina mambo mengi inahitaji wataalamu wengi hivyo sekta binfsi inatakiwa kuhakiskisha wafanyabiashara wana uwezo wa utafuta masoko ambayo tayari yapo huru huku waktumia teknolojia,” alieleza.

Hata hivyo aiwashauri watanzania waweze kuchangamkiafursa na kuweza kuridhia mikataba huu na kuungana na mataifa mengine barani afrika katika kufanya biashara na kuwa wamoja.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Biashara na ukuzaji masoko Khamis Mikidadi alieleza kwamba, wakati uwefika kwa watanzania kwa ujumla kuridhia mkatab huo ili wafanyabiashar wa ndani waweze kunufaika na uweo wa soko huru barani afrika.

Aidha aliwaasa wananchi wa Tanzania kuchangamkia fursa za masoko ambao zinapatikana kupitia soko la pamoja barani afrika.

“Ninacho waambia wananchi kwaba wawe tayari kuzalisha, wawe tayari kusafirisa bidhaa zao ambapo huko kwenye sokoa la pamoja ndipo kwenye masoko ya uhakika,” aleleza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jumuiya ya wafanyabiashara Zanzibar, Hamad Hamad alisema kuwa kupitia mkutan huo Jumuiya ya wafanyabiashara na sekta nzima binafsi imepata uwelewa wa kutosha namna bora ya kushiriki katika soko hilo.

“Kama tunayofahamu uwa Tanzania bado haijaridhia ila ipo katika hatua za mwisho za kuingia katika soko huru la afrika, sisi kama sekta binafsi tunajiandaa kungia kama wenzetu ambao tayari wameshaingia na kunufaika,”alisema.

Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Zanzibar Ali Amour alisema kuwa endapo Tanzania ikiingia kikamilifu katika soko hilo kuna faida kubwa kwa wananchi wake wanaweza kufaidika ambazo zitasaidia katika kuongeza kipato kwa wananchi.


Comments