Wakamatwa kwa kutoa chanjo bandia Uganda


 


Washukiwa wadanganyifu wawili wamekamatwa nchini Uganda kwa kutoa chanjo bandia za Covid19.

Maafisa wanasema kwamba bado haijulikani ni nini kilikuwa kwenye chanjo ambazo walitumia lakini wanafanya uchunguzi juu ya dawa hiyo.

Inaaminika kuwa washukiwa hao wawili huenda waliwachoma chanjo watu mpaka 800 katika makampuni binafsi ambayo waliandaa chanjo kwa ajili ya wafanyakazi wake.

Kitengo cha ufuatiliaji kimesema kilipata tetesi kupitia viongozi wa ngazi za chini kuwa wawili hao walizunguka katika maeneo ya Kampala, wakidai ni wafanyakazi wa idara ya afya kutoka hospitali za mwanzo mjini humo.

Chanjo ya corona nchini Uganda ni bure, na zinapatikana katika vituo vya umma na binafsi. Zaidi ya watu 856,000 mpaka sasa wamepatiwa chanjo.

Comments