POLISI Mkoani Mtwara imikamata watu 15 kwa tuhuma za kuuza viuatilifu feki vya salpha na vya maji ambavyo vinatumika kudhibiti magonjwa ya zao la korosho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigadia Jenerali Marco Gaguti amewaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa watu hao walikamatwa na viuatilifu vya salpha tani 84.3 na vya maji tani 292 ambavyo vimeisha muda wake wamatumizi.
“Watu hao walikamatwa katika zoezi lilofanywa na jeshi la polisi mkaoni hapa baada ya kupata taarifa za awali za uwepo wa viuatilifu feki katika baadhi ya maduka maeneo mbalimbali Mtwara,” amesema.
Kufuatia hatua hiyo, Gaguti ameelekeza jeshi la polisi kukamilisha taratibu za kipolisi na watuhumiwa kufikishwa haraka kwenye vyombo vya sheria.
Pia ameagiza kufungwa kwa maduka pamoja na maghala ambayo yalihusika katika hujuma hiyo ya kuuza na kuhifadhi viuatilifu ambavyo vimeisha mda wake mpaka pale kesi ya msingi itakapokamilika.
Pia Gaguti amewaomba wananchi wa pamoja na wakulima kuwa waangalifu na kufuatilia kuhakikisha ubora wa viuatilifu na madawa mengine wayanyotumia katika kudhibiti magonjwa ya korosho.
“Ninawaomba wa Mtwara haswa wakulima kuwa macho wanapotafuta viuatiliu na madawa ya mikorosho, wawe makini kuangalia na kufuatilia ubora wa madwa wanayonunua na kutoa taarifa mapeam ili tuweze kukabiliana na uwepo wa madwa feki,” amesema.
Viautilifu hivyo vilikamatwa katika maeneo ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Tandahimb, Newala na Nanyumbu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Mark Njera amesema uchunguzi wa awali ulibaini kuwa watuhumiwa hao walitumia mbinu za kuwahadaa wakulima kwa kuwaambia kuwa wameruhusiwa na mamlaka husika kuuza hivyo viuatilifu pamoja na kuwa vimeharibika huku wakiwaambia kuwa havina tatizo.
Pia watuhumiwa hao walitumia barua ambayo walidai wamepewa na mamlaka husika ambazo ziliwapa idhini kuuza hivyo viuatilifu feki pia walitumia nyaraka za kughushi kuonyesha kwamba wamepewa idhini na mamlaka husika kuuza viuatilifu hivyo.
Comments
Post a Comment