Tahadhari yatolewa kuhusu kitisho cha shambulizi la kigaidi Kabul



Nchi za Magharibi zimewatahadharisha Raia wake kuondoka mara moja katika uwanja wa ndege wa Kabul na kufuatia tishio la shambulizi la kigaidi, tayari Ubalozi wa Marekani mjini Kabul umewataka Raia wake walioko katika malango ya Abbey, Mashariki na Kaskazini kuondoka mara moja.

Australia kupitia Wizara yake ya mambo ya Nchi za nje imesema kuna kitisho kikubwa cha kufanyika shambulizi la kigaidi ambapo pia Uingereza imetoa tahadhari kama hiyo kwa Raia wake.

Waziri wa Vikosi vya Ulinzi vya Uingereza James Heappey amesema kitisho hicho ni cha kuaminika na ni hatari, tahadhari hii imetolewa wakati maelfu ya Waafghani na Raia wengine wa kigeni wakiwa na matumaini ya kupandishwa kwenye Ndege za kuwaondoa nchini humo.

Comments