Muwekezaji wa kiwanda cha chai Lupembe apokwa kiwanda na Mahakama, Chaludishwa kwa wakulima




Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mahakama kuu ya Tanzania imefutilia mbali kesi no 193 ya mwaka 2008 iliyokuwa imefunguliwa na muwekezaji wa kiwanda cha chai Lupembe dhidi ya wakulima wa chai waliyochini ya mwanvuli wa chama kikuu cha ushirika tarafa ya Lupembe MVYULU kwa kufanya uvamizi wa kiwanda na kukiuka taratibu za mkataba wa mauziano ya kiwanda.

Kesi hiyo iliyolindima kwa zaidi ya miaka 14 tangu ifunguliwe huku kila upande ukiamini kuwa sahihi kwa unachokiamini na kukisimamia na kupelekea viongozi wakubwa wa serikali akiwemo waziri mkuu,waziri wa kilimo na katibu mkuu kufika kwa nyakati tofauti kusuruhisha mgogoro,Hatimae imefika mwisho baada ya september 24 mahakama kuu ya jijini Dar es salaamu kutupilia mbali kesi hiyo na kisha kutamka MVYULU kuwa mmiliki halali wa kiwanda hicho. 

Akizungumza na wananchi na viongozi kutoka kata zote za jimbo la Lupembe mbunge wa jimbo hilo Edwin Swale amesema hakuna tena kesi dhidi ya Muwekezaji na wananchi wa Lupembe kwa kuwa mahakama imeamuru kesi hiyo kufutwa baada ya kuifatilia kwa zaidi ya miaka 17 na kwamba kilichobaki ni kukabidhiwa tena wananchi baada ya uhakiki.

“Kesi namba 94 ya mwaka ya mwaka 2016 ambayo ambayo ili lufaa iliyokuwa mahakama ya Lufani ikihusisha wakulima wa chai Lupembe na muwekezaji imekwisha na mahakamni hakuna tena ile kesi”alisema Swale

“Jamabo la pili hukumu ya mahakama kuu iliyotamka watu wa Lupembe kulipa mabilioni ya fedha ambayo ni hukumu ya kesi namba 193 ya mwaka 2008 imefutwa haipo tena na tuliyokubalina sasa kiwanda cha wananchi wa Lupembe baada ya kufanyiwa ukaguzi mkubwa kinakabidhiwa rasmi kwa wananchi wa tarafa ya Lupembe aliongeza Swale

Nae Wlfred Swale ni mwenyekiti wa muungano wa vyama vya ushirika tarafa ya Lupembe Mvyulu akiweka bayana mchakato wa kesi na msimamo wa wakulima wa chai Lupembe anasema chanzo cha mgogoro wa umiliki wa kiwanda hicho ni serikali kwasababu iliuza hisa za wakulima kwa muwekezaji wakati wao ndiyo waliokinunua kwa mzungu aliejulikana kwa jina Wiliamson kwa kukatwa fedha za majani 

“Mgogoro wa kiwanda kile una miaka 17 kutoka mwaka 2004 mpaka tarehe 24 ijumaa ya mwezi wa 9 ndio uamuzi umefanyika,tulikwa tumeshindwa kesi tukaapeal kwenye mahakama ya rufaa tumeendesha kwa milolongo mingi na kesi ilikuwa kwasababu serikali imeuza hisa za wakulima 70 tukabakiwa na hisa 30”alisema Wilfred Swale 

Ujio wa taarifa za kurejeshwa kwa kiwanda cha Lupembe kwa wakulima wa chai walio chini ya mwamvuli wa MVYULU kumepokelewa kwa hisia na wakazi wa Lupembe ambapo mzee Gerson Mwavika na Elida Malekela wanasema walianza kulisusa zao la chai kwasabau ya kunyang'anywa kiwanda chao walichokatwa baba na mama zao fedha za majani ya chai na kahawa ili kukinunua kwa mzngu.

“Tulikuwa tunapambana kwasababu hata mimi ni mmoja kati ya wale ambao tulikuwa tunatoa fedha kupitia chai kidogo,kahawa na pareto zilizokuwa zinakatwa kwenye ushirika na ndio ushirika ulinunua kiwanda hiki kwa hiyo sisi tulikuwa na haki”alisema Gerson Mwavika

“Tulichangia fedha kutoka kwa baba zetu na sisi pia tulipoingia ushirika tulichangia kwa hiyo kwa sasa tunahitaji mwekezaji ambaye anatuthamini wakulima”alisema Elida Malekela

Comments