NATO yaimarisha doria mpaka wa Kosovo na Serbia



Vikosi vya Jumuia ya Kujihami ya NATO vimeongeza doria kwenye mpaka wa kaskazini karibu na Serbia. 
 
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Serbia kupeleka vifaru vya jeshi kwenye mpaka na wananchi wa Serbia walioko Kosovo kupinga uamuzi wa serikali ya Kosovo kuhusu namba za magari. 
 
Serbia haiitambui Kosovo wala namba zake za magari na inawataka madereva kutoka Kosovo kuondoa namba hizo na kununua namba za muda wakati wanaendesha magari yao Serbia.
 
 Vivyo hivyo, Kosovo iliamua kuchukua hatua kama hizo, ikiwataka madereva wa Serbia walioko Kosovo kulipa euro tano ili kupata namba za muda wakiwa Kosovo.
 
 Waserbia walioko kaskazini mwa Kosovo kwa hasira walipinga hatua hiyo wiki iliyopita na walizuia barabara na maeneo mawili ya mipaka kuelekea Serbia. 
 
Kwa upande wake Serbia ilipeleka vifaru na ndege za kijeshi zilizunguka eneo la mpaka.

 

Comments