Tetesi za soka kimataifa



Borussia Dortmund wanafikiria kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Manchester United Anthony Martial, 25, ikiwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 21, ataondoka katika klabu hiyo msimu wa joto. (Sport1 - in German)

Barcelona na Real Madrid watakua miongoni mwa klabu zinazomwania kiungo wa kati wa Leicester Youri Tielemans, 24, ikiwa kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji atauzwa, msimu ujao. (Athletic - subscription required)

West Ham wanashughulikia mpango wa kumsajili kiungo wa Juventus Weston McKennie, 23, na mazungumzo tayari yamefanyika juu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani. (Football Insider)

Winga wa zamani wa Bournemouth Arnaut Danjuma, 24, anafuatiliwa kwa karibu na Liverpool baada ya Mholanzi huyo kuanza msimu vizuri katika klabu yake mpya ya Villarreal. (Voetbal International - in Dutch)

Liverpool wamekuwa wakimfuatilia kiungo wa kati wa Porto Mcolombia Luis Diaz, 24. (Independent - subscription required)

Chelsea na Liverpool zinamnyatia winga wa Newcastle na Ufaransa Allan Saint-Maximin, 24. (Calciomercato via Express)

Tottenham huenda wakasubiri hadi msimu ujao badala ya Januari kabla ya kujaribu kumuuza tena Dele Alli,25, ikizingatiwa thamani ya kiungo huyo wa kati wa England ilivyoshuka. (Football Insider)

Barcelona wamepokea ofa kutoka kwa kampuni ya Dubai ya kununua deni la klabu hiyo la euro bilioni 1.5 (£1.2bn). (8tv via Mirror)

Barca wameungana na Bayern Munich katika kinyang'anyiro cha kumsaka winga wa Ajax Mbrazili Antony, 21. (Sport - in Spanish)

Chelsea na Bayern Munich kwa sasa hawana mpango wowote wa kubadilishana wachezaji kati ya winga wa Marekani Christian Pulisic, 23, na winga wa Bayern Mjerumani Leroy Sane,25, licha ya uvumi unaoendelea. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Roma Jose Mourinho anataka kumleta kiungo wa kati wa Tottenham na Ufaransa Tanguy Ndombele, 24, katika klabu hiyo. (Calciomercato via FourFourTwo)

Real Betis wameanza mazungumzo ya kurefusha mkataba wa mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir, 28. (Marca - in Spanish)

Nahodha wa Tottenham na kipa wa Ufaransa Hugo Lloris, 34, amemuomba kocha Nuno Espirito Santo kuwa na subira na kumpatia muda aweke mambo sawa katika klabu hiyo and to give him time to make things work at the club. (Evening Standard)

Real Madrid wanamtaka kiungo wa Inter Milan Alessandro Bastoni, ijapokuwathamani ya sasa mlinzi huyo wa Italia mwenye miaka 22, inakadiriwa kuwa euro milioni 60 (£51.7m). (Mundo Deportivo - in Spanish)

Real pia wanataka kumsajili nahodha wa Ivory Coast na kiungo wa zamani wa Tottenham Serge Aurier, 28. (Star

Comments