Uchaguzi wa Haiti waahirishwa kwa muda usiojulikana



Uchaguzi na kura ya maoni kuifanyia mabadiliko katiba zilizopangwa kufanyika katika miezi ijayo nchini Haiti, imeahirishwa kwa muda usiojulikana. 
 
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya wajumbe wa tume ya uchaguzi kufukuzwa na kuiingiza nchi hizo katika hali ya mkwamo zaidi. 
 
Tangu kuteuliwa kwao Septemba 2020, wajumbe tisa wa Baraza la Muda la Uchaguzi, CEP wamekuwa wakikosolewa na upinzani na umma. Wajumbe hao waliteuliwa na rais aliyeuawa mwezi Julai, Jovenel Moise. 
 
Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry jana alitangaza kuwa anawafuta kazi wajumbe hao na anajiandaa kuteua baraza jipya, lakini hakutangaza tarehe ya kufanya hivyo.
 
 Awali, duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais na wabunge, pamoja na kura ya maoni kuifanyia mabadiliko katiba ilipangwa kufanyika Novemba 7. Duru ya pili ilipangwa kufanyika Januari 23, mwaka 2022.

 

Comments