Dar es Salaam yaongoza kimikoa matokeo Darasa la Saba 2021


Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi 2021 na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.89

Akitangaza matokeo hayo jana Jumamosi Oktoba 30, 2021 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde  ametaja katika mpangilio wa mikoa Dar es Salaam imeongoza kitaifa kwa asilimia 96.54 ikifuatiwa na Iringa iliyopata asilimia 91.01, Mbeya asilimia 88.14, Arusha asilimia 88.00, Njombe asilimia 86.90, Kilimanjaro asilimia 86.74, Katavi asilimia 86.65, Lindi asilimia 86.32, Simiyu asilimia 85.52 na Pwani asilimia 84.91.

Mpangilio wa halmashauri unaonyesha Ilala CC inaongoza kwa ufaulu wa asilimia 98.52 ikifuatiwa na Arusha CC asilimia 98.50, Kinondoni MC asilimia 98.35, Moshi MC asilimia 97.53, Mwanza CC asilimia 97.40, Iringa MC asilimia 97.28, Ilemela MC asilimia 96.70, Mafinga TC asilimia 96.61, Kigamboni MC asilimia 96.29 na Ilala asilimia 96.28.

 

Comments