Hasheem Thabeet apata timu mpya nchini Taiwan


Mcheza kikapu nyota wa kimataifa wa Tanzania, Hasheem Thabit amesajiliwa kwenye klabu mpya iitwayo Tainan TSG inayoshiriki ligi Kuu ya kikapu ya nchini Taiwan barani Asia.

Usajili huo umezima fununu za nyota huyo kurejea kwenye Ligi kuu ya Kikapu ya Nchini Marekani ‘NBA’ ambapo aliichezea miaka kumi iliyopita kwenye vilabu vya Memphis Glizzlies na OklahomaCity Thunder.

Hasheem mwenye umri wa miaka 34 kwasasa, si mgeni na mazingira hayo kwani msimu uliopita aliichezea timu ya Hsinchu JKO Lioneers ya nchini Taiwan na kuibuka kuwa mlinzi bora wa msimu kwa mwaka 2020, mchezaji mwenye rebound nyingi na blocks nyingi.

Ikumbukwe kuwa Hasheem aliichezea timu ya Savio ya nchini Tanzania na kuisaidia kushinda ubingwa wa Ligi kuu ya Mkoa wa Dar es Salaam ‘RBA’ mbele ya timu ya ABC na kuibuka kuwa MVP wa fainali za RBA 2021.

Uamuzi wa kurejea nchini Tanzania ulisababishwa kwa kiasi kikubwa na ugonjwa wa Covid-19 uliopelekea ligi ya Taiwan isitambe hivyo aliitumikia timu ya Savio kujiweka fiti huku kukiwa na fununu kuwa alikuwa akiangalia uwezekano wa kurejea NBA.

Comments