Kiongozi wa Kianglikana 'anahofu' na muswada wa kupinga wapenzi wa jinsia moja Ghana



Askofu mkuu wa Canterbury, ambaye ni kiongozi wa Waanglikana kote duniani, amesema kuwa ana “hofu kubwa” ukuhusu muswada mpya wa sheria unaopendekezwa nchini Ghana, ambayo inaweza kuweka adhabu kubwa kwa jamii ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia LGBT.

Muswada huo unajadiliwa katika bunge, huku ukitarajiwa kupigiwa kura katika siku chache zijazo.

Muswada huo unaungwa mkono na Kanisa la Kianglikana la Ghana-licha ya makubaliano ya makasa yote kwamba hayataunga mkono sheria zenye ubaguzi.

Muswada huo unataka kuongeza kuongeza adhabu ya kifuno cha jela kwa hadi miaka kumi na kuwalazimisha baadhi ya wapenzi wa jinsia mojakufanyiwa matibabu ambapo, majaribio ya kubadilisha jinsia zao yatafayika.

Uvaaji wa mavazi na kuonyesha wazi upendo wa mapenzi ya jinsia moja hadharani litakuwa ni kosa linaloadhibiwa kwa faini au kifungo.

 

Comments