Mbuga ya wanyamapori ya Serengeti ndio bora zaidi Afrika


Mamlaka ya Tuzo ya dunia ya safari(WTA)imeitangaza Mbuga ya wanyama ya Serengeti nchini Tanzania kama mbuga ya wanyama inayoongoza barani Afrika mwaka 2021.

Serengeti imekuwa ni mbuga ya wanyama inayoongoza Afrika kwa mara ya tatu katika mwaka 2019, 2020 na 2021, imesema taarifa iliyotolewa na mamlaka ya Mbuga za Wanyama nchini Tanzania.

Mbunga nnyingine zilizoteuliwa katika Mbuga za wanyama zinazoongoza ni pamoja na hifadhi ya wanyama ya kalahari-Central Game Reserve Botwana, Mbuga ya wanyama ya Elosha nchini Namibia, Kidepo Valley National Park Uganda; Kruger National Park ya Afrika Kusini na Hifadhi ya wanyama ya Maasai Mara nchini Kenya.

Serengeti yenye ukubwa wa kilomita za mraba 14,763, ni maarufu kwa kuwa na aina mbali mbali za wanyama, ndege na mimea wa spishi mbali mbali.

Aina 70 za spishi za wanyama wakubwa na 500 za ndege hupatikana katika mbuga hii iliyopo Tanzania.

 

Comments