Papa ataka jibu 'kali' kwa mabadiliko ya hali ya hewa katika mahojiano na BBC


Katika ujumbe uliorekodiwa mahsusi kwa ajili ya BBC, Papa Francis ametoa wito kwa viongozi wa dunia wanaokutana juma lijalo katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa mjini Glasgow kutoa "majibu ya ufanisi" kwa dharura ya mazingira na kutoa "tumaini thabiti" kwa kizazi kijacho.

Akizungumza na BBC kutoka mjini Vatcan kwa ajili ya kipindi cha BBC Radio 4's Thought for the Day, Papa alizungumzia kuhusu mizoz, ikiwa ni pamoja na janga la Covid-19, mabadiliko ya hali ya hew ana matatizo ya uchumi, na kuitaka dunia kuyashugulikia kwa maono na maamuzi makali, ili "kutopoteza fursa" zinaoletwa na changamoto zilizopo.

"Tunaweza kukabiliana na mizozo hii kwa kuacha utengeno, kulindana na unyanyaji," alisema Papa, "au tunaweza kuona ndani yao fursa halisi kwa ajili ya mabadiliko."

Alielezea juu ya haja ya "ushirikishwanaji wa wajibukwa ajili ya dunia yetu ", akiongeza kuwa "kila mmoja wetu- yeyote na popote pale alipo-anaweza kutoa mchango wake katika kubadili jinsi tunavyoshugulikia tisho lisilotarajiwa la mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu wa nyumba zetu."

Kwa miaka sita mfulurizo viongozi wa dunia wamekuwa wakikutana na sasa wanajiandaa kukutana katika mji wa Glasgow kwa ajili mkutano wa hali ya hewa, unaofahamika kama, COP26.

 

Comments