RC Mwanza atoa siku tatu kwa Muhandisi wa mkoa na timu yake kuandaa maeneo ya Machinga



Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza mhandisi Robert Gabriel  ametoa onyo kwa  baadhi ya  watu ambao wameanza utapeli kwa wamachinga kwa kuwadai fedha ili kuwapatia maeneo ya kufanya biashara.

Mhandisi  Gabriel amemtaka mhandisi wa mkoa na timu yake kuongeza nguvu kwenye timu ya jiji ili waweze kuandaa maeneo kwa machinga ambao hawajapata maeneo

Hayo aliyasema jana ofisini kwake wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani hapa.

Amesema timu ya jiji la Nyamagana wanaoratibu shughuli za   kuwapanga wafanyabiashara maarufu kama machinga kuhakikisha wanamaliza kazi hiyo kwa nataka.

Amesema anapokea maombi ya machinga wanaofanya biashara zao kwenye maeneo ya barabara ya soko la Buhongwa kuondoka maeneo yasiyo rasmi ifikapo Novemba 10 mwaka.

"Ifikapo Novemba 10 maeneo yatakuwa yameshakamilika kwenye ujenzi wa climbs kwenye maeneo rasmi yaliyopangwa kwa ajili ya kufanya biashara.

Hata hivyo amesema serikali imetoa maeneo bure ili wafanyabiashara hao waweze kujitafutia kipato iwapo.

"Nikibaini kuna watu,kikundi kinawaomba fedha ili mpate maeneo toeni taarifa kwa uongozi ilu tuweze kuchukua hatua za kisheria.

Amelitaka shirika la umeme nchini kuhakikisha wanafanya taratibu za kuweka umeme na kuainisha maeneo ambayo wafanyabiashara hao
 ili waweze kuweka huduma hiyo kwenye vizimba vyao.

Comments