Shahidi kesi ya kina Mbowe ashindwa kufika mahakamani, yaahirishwa



Mahakama Kuu (Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi), imeahirisha kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu baada ya shahidi wa tatu wa Jamhuri kushindwa kufika mahakamani.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Robert Kidando ameeleza hayo leo, Oktoba 28, 2021, muda mfupi baada ya shahidi wa pili katika kesi hiyo, Justine Kaaya, kumaliza kuhojiwa na mawakili wa utetezi.

"Mheshimiwa Jaji, shahidi tuliyetarajia kuja kutoa ushahidi hajafika na leo ndio anasafiri kuja, hivyo tunaomba ahirisho la kesi hii hadi kesho, Oktoba 29, 2021" amedai wakili Kidando mbele ya Jaji Joachim Tiganga.

Baada ya kutoa maelezo hayo, upande wa utetezi ulioongozwa na Peter Kibatala haukuwa na pingamizi kwa ombi hilo.

Jaji Tiganga ameahirisha shauri hilo hadi kesho saa tatu asubuhi ambapo shahidi huyo atatoa ushahidi.

 

Comments