Wamiliki wa vyombo vya moto jitokezeni kwa ukaguzi



Na Maridhia Ngemela, Mwanza

Ikiwa ni wiki ya nenda kwa usalama barabara wamiliki wa vyombo vya moto wameshauriwa kujitokeza kwa ajili ya kukaguliwa magari yao ili kuepukana na ajali za barabarani.

Hayo yamesemwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Ramadhani Ng'anzi alipokuwa katika zoezi la ukaguzi wa magari katika kituo cha mabasi buzuruga mkoani Mwanza.
 
Kamanda Ng'anzi amesema kuwa,kila gari litakalo kaguliwa litapewa stika ya ukaguzi ikiwa ni alama ya utambuzi ili kuepukana na usumbufu unaoweza kujitokeza barabarani.

"Kuanzia leo tutawakamata wanaoweka vimulimuli kwenye magari na kushitakiwa kwani niukiukwaji wa sheria na wale madereva wanaoendesha magari bila kuwa na leseni tutawakamata pia na gari isiyokuwa na stika itakamatwa kwahiyo niwaombe wamiliki wa magari wajitokeze kwa wingi kwaajili ya ukaguzi na lengo letu sisi ni kuwa na alama ya sifuri kwa ajali za barabarani na kauli mbiu ya mwaka huu ni mkinge mwenzako na ujikinge wemwenyewe ilikuweza kuepusha ajali za barabarani amesema Kamanda Ng'anzi.

Mwenyekiti wa baraza la usalama barabarani mkoa wa Mwanza Fednandi Chacha amesema wamejipanga vizuri kumaliza ajali ambazo zinatokea barabarani wananchi wasipote njia ya mkato kuchukua stika bila gari kukaguliwa kwani lengo ni kuwa na vyombo vilivyo salama.

Miongoni mwa wamiliki wa magari wakipata nafasi ya kuzungumza katika zoezi hilo ni slivesta Wambura kutoka kampuni ya Afrika raha amesema kuwa wamiliki wa magari wajitokeze kwa wingi watoe ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuepukana na ajali.

Naye ispekta Issa  Hamidu  ocs kutoka kituo cha buzuruga stendi amesema elimu atakayotoa ni kuhakikisha madereva wanaelewa umuhimu wa zoezi la ukaguzi wa magari.

"Elimu nitakayotoa ni kwa madereva na wamiliki wahakikishe magari yao ya nakaguliwa na kupatiwa stika kama afande alivyoeleza kuwa magari ya biashara ni shilingi elfu tano,madogo elfu tatu na pikipiki shilingi elfu moja kamanda ametoa namba hapa mkiona mtu anawatoza fedha ambayo haiyendani na maelekezo hayo mpige simu moja kwa moja kwa Kamanda ili kurahisisha zoezi hili lengo letu sisi nikuona mkoa wetu hauna ajali kabisa amesama Inspekta hamidu.

Kwa upande wake mkaguzi  wa polisi kutoka Wilaya ya Sengerema DTO Buhembele  amesema kuwa sheria ya kufungua 39  kinawataka wamiliki wa vyombo vya moto kuwasafirisha abiria wakiwa salama

 DTO Buhembele Ametoa rai kwa wananchi hususani abiria kuacha kuchochea madereva kuendasha kwa mwendokasi ambao unaweza kuhabarisha maisha yao na watembelee mabanda yaliyopo Wilayani hapo kwa lengo la kupatiwa elimu ili kuzuia ajali ambazo hujitokeza mara kwa mara kwa uzembe wa baadhi ya madereva na wamiliki wa magari kutotii sheria.


Kwa upande wa Wilaya ya Nyamagana ACP Fedrick mpolo DTO Nyamagana amesema kuwa watahakikisha chimbo cha moto kinachoingia barabarani kinakuwa salama  na magari ya wanafunzi watayasimamia kuhakikisha usalama wao ili kuokoa maisha ya Watanzani amewaomba wamiliki wa vyombo hivyo katika wiki hii ya nenda salama barabarani.

Comments