Vidonge vya Pfizer vinaweza kutibu corona kwa 89%



Kidonge cha majaribio cha kutibu Covid kilichotengenezwa na kampuni ya Pfizer nchini Marekani kinapunguza hatari ya kulazwa au kifo kwa 89% kwa watu wazima walio hatarini, matokeo ya majaribio ya kliniki yanapendekeza.


Dawa za- Paxlovid - inakusudiwa kutumika mara tu mtu anapopata dalili kwa wale ambao wako hatari kubwa ya ugonjwa huu.


Maelezo haya yamekuja siku moja baada ya mamlaka ya dawa nchini Uingereza kuthibitisha tiba inayofanana na hiyo kutoka Merck Sharp na Dohme (MSD).


Pfizer inasema imeacha kufanya majaribio mara tu walipopata matokeo chanya ya dawa hiyo.


Uingereza imeagiza dozi 250,000 za dawa za Pfizer na dawa 480,000 za vidonge vya MSD molnupiravir.


Dawa hizi mgonjwa anakunywa vidonge vitatu kwa siku kwa kipindi cha siku tano.

Comments