Manchester City inakusudia kumsajili kiungo Mholanzi Tijjani Reijnders (26) kutoka AC Milan, ambao watamuuza kama ofa ya zaidi ya pauni milioni 57 itatolewa (Telegraph)
Uongozi wa Manchester United hauna mpango wa haraka wa kumfukuza kocha wao Ruben Amorim (Talksport)
Winga wa Colombia Luis Diaz (28) ameahidi kusalia Liverpool licha ya kuhusishwa awali na Barcelona. (Express)
Real Madrid bado haijatoa ofa rasmi kwa Liverpool kumsajili beki wa kulia Trent Alexander-Arnold (26), ingawa walimuulizia wiki iliyopita kwa ajili ya Kombe la Dunia la Klabu mwezi ujao. (Sky Sports)
Liverpool inaweza kumchukua Jeremie Frimpong (24) wa Bayer Leverkusen na mholanzi, ambaye ana kipengele cha kuuzwa kwa pauni milioni 29.4-33.6. (Sky Germany)
Beki wa Newcastle Sven Botman (25) anataka kubaki kwenye klabu hiyo licha ya kuvutiwa na Paris St-Germain. (The I)
Napoli wamefanya mazungumzo na upande wa Kevin de Bruyne kuhusu uwezekano wa kumsajili bure msimu wa joto atakapomaliza mkataba na Manchester City. (Sky Switzerland)
Atletico Madrid wanapanga kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu usajili wa winga wa Brazil Antony (25), ambaye kwa sasa yupo kwa mkopo Real Betis, huku Juventus na Villarreal pia wakimhitaji. (Football Espana)
Real Madrid wanavutiwa na mpango wa kumrejesha beki wa kushoto wa Ufaransa Theo Hernandez (27) kutoka AC Milan, miaka sita baada ya kuondoka klabuni hapo. (Calciomercato
Comments
Post a Comment